Siku zote msaliti hakubali kuona akisalitiwa, hata kama kukiwa hakuna dalili ya kufanyiwa hivyo. Hawezi kuwa na amani asilani, daima huhisi atageukwa... > Lire la suite
Siku zote msaliti hakubali kuona akisalitiwa, hata kama kukiwa hakuna dalili ya kufanyiwa hivyo. Hawezi kuwa na amani asilani, daima huhisi atageukwa kama alivyogeuka mwingine. Hawezi kustahimili kufanyiwa jambo alilomfanyia mwingine, maumivu yake huyajua. Ndiyo hapo Saibah binti wa Sultan Zuad aliyemsaliti mumewe, mpaka akaja kufumwa na kijakazi kitandani. Bado alifikia kumwonesha jeuri ya waziwazi na si kukubali alikosea, kisa nyumba waliyoishi ni kwao. Mpaka bwana yule aliamua kuondoka na kumwachia nyumba, na akabaki akikaa nje akiendelea na majukumu yake kama Mkuu wa majeshi wa himaya. Aliachwa solemba na kijakazi yule, akaja kujua mume ni wa muhimu. Wakati ambao yupo vitani. Alipokuja kurudi ni majeruhi na hana fahamu, muda huo napo mwanamke aliyependwa na mumewe anarejea kumjulia hali. Ndiyo hapo sasa wasiwasi wa penzi wa msaliti unapoibuka